• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI. PILLY KITWANA AWATAKA MAAFISA ELIMU KATA NA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI KUSIMAMIA VIZURI MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: July 9th, 2025


Na: Nuru Mangalili – Ifakara Tc  , Habari 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara  Bi. Pilly Kitwana amewataka Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari kuhakikisha wanasimamia vizuri Miradi ya Maendeleo katika Shule zao.

Hayo ameyasema tarehe 9 Julai 2025 wakati alipofanya Kikao na Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi  zilizopo Halmashauri ya Mji Ifakara.

“Kila mmoja atekeleze wajibu wake, kama umeletewa miradi kwenye eneo lako hakikisha kwa kufuata taratibu na miongozo miradi ikamilike kwa wakati . Huu ni mwaka mpya wa Fedha, kuna fedha zitaletwa kwaajili ya Miradi  muhakikishe mnakua wasimamizi wazuri wa Miradi hiyo”. Alisema Bi. Pilly Kitwana

Aidha Bi. Pilly Kitwana aliwasisitiza  Waratibu hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata taratibu , miongozo, sheria na maadili ya Utumishi wa Umma , kuhakikisha wanaongeza ufaulu wa wanafunzi na Mahusiano mazuri kazini.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri  ya Mji Ifakara Bw. Folkward Mchami alisisitiza Waratibu hao wa Elimu kuhakikisha hakuna Mwanafunzi atakaye pata Divisheni Ziro katika Halmashauri ya Mji Ifakara.

“ Tunampango wa kufuta Divisheni Ziro, katika kila Shule, hivyo Walimu tuhakikishe wanafunzi wote wanafaulu kwa kuondoa utoro mashuleni  na kuhakikisha walimu wanafundisha vipindi vyote kwa weledi”. Alieleza Bw. Mchami

Bi. Pilly Kitwana alisiskiliza changamoto na kero mbalimbali za Waratibu hao wa Elimu na kuzipatia ufumbuzi

.

Wakati huohuo Bw. Bonaventure Nyoni Afisa Elimu Kata ya Mkula alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana kwa Kikao hicho na kuahidi kuondoa Ziro Mashuleni Pamoja na kusimamia vizuri miradi.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani