• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

MKURUGENZI IFAKARA MJI AWAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA.

Posted on: May 28th, 2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana amewahimiza Wananchi  wa Halmashauri ya Mji Ifakara na maeneo ya jirani  kujitokeza kwa wingi kupata huduma za  Matibabu ya Kibingwa  kutoka kwa Madaktari Bingwa waliotoka nchini Italia wakishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisko - Ifakara  kwaajili ya kutoa huduma za Matibabu ya  Upimaji wa Magonjwa ya Masikio ,  Pua na Koo . Mdomo sungura, Matende na mabusha , vidonda n.k

Hayo ameyasema leo tarehe 28 Mei ,2025 wakati akizindua  huduma za Matibabu ya Kibingwa katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisko zinazotolewa na Madaktari hao waliotoka nchini Italia  kwa kushirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisko Ifakara.


Aidha  alimshukuru  Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya Taasisi za Dini na Serikali ambayo yanapelekea kuboresha utolewaji wa huduma kwa jamii.


Wakati huohuo Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya  Mtakatifu Fransisko Ifakara Fr. Dkt . Winifridi Gingo alisema Hospitali hiyo ya Rufaa ya  Mkoa ya  Mtakatifu Fransisko hupokea Madaktari hao kila mwaka kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa kwa Wagonjwa hao ambapo mara baada ya kumaliza huwaachia ujuzi , uzoefu na vifaa  Madaktari Bingwa wa Hospitali hiyo.

" Huduma hizi zimeanza kuanzia leo tarehe 28 /5/2025 Hadi tarehe 11/6/2025  na uchunguzi wa magonjwa haya ni bure na Matibabu yake yanafanyika kwa punguzo la bei" . Alisema  Fr. Dkt. Gingo


Kwa upande wake Kiongozi wa Madaktari  Bingwa kutoka Bologna - Italy Dkt. Actovia Vichi alishukuru kwa Mapokezi mazuri kwa Ofisi ya Mkurugenzi  kwa kushirikiana na  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisko na kuahidi kuwahudumia vizuri   kwa Wagonjwa wote  watakaofika hapo Kupata Matibabu.

Huduma hizo zinatolewa kwa Kushirikiana na  Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtakatifu Fransisko -Ifakara.





Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani