• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

MAFUNZO KWA WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI (BVR) KWA AJILI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU 2025.

Posted on: February 26th, 2025

Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki (BVR)  Jimbo la Kilombero Februari 26 ,2025 wamepatiwa Mafunzo  kuelekea zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia 1-7 Machi 2025 katika Vituo mbalimbali ndani ya Kata zote 19 za Jimbo la Kilombero.


Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wahusika kupata ujuzi wa kina kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya BVR, usimamizi wa taarifa za wapiga kura, na kuhakikisha usahihi wa taarifa ili kuepusha dosari zinazoweza kuathiri mchakato wa uchaguzi. Vilevile kuhimiza uadilifu, uwajibikaji, na weledi katika kutekeleza majukumu yao.


Aidha, Mratibu wa Uandikishaji wa  Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Tesha  aliwasisitiza Washiriki hao kuwa wasikivu na Makini katika Mafunzo hayo Ili wakafanye Kazi kwa weledi katika Vituo watakavyokwenda kufanyia Kazi  na kuhakikisha kila mmoja  anatunza vizuri  vifaa hivyo vya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura

.

" Hili ni suala muhimu kitaifa muhakikishe mnaongeza umakini na Uadilifu wa hali ya Juu, mkazingatie Sheria , kanuni na weledi katika zoezi hili. " Alieleza Bw. Tesha.


Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo alikua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana ambaye aliwataka Wasaidizi hao kuhakikisha wanafuta yale watakayofundishwa katika semina hiyo Ili zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura lifanyike kwa weledi.


Jumla ya Washiriki 634 wamepatiwa Mafunzo hayo ya siku mbili  yaliyoanza leo tarehe 26 Februari 2025 na kuhitimishwa hapo kesho tarehe 27 Februari 2025.







Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani