MADIWANI WILAYA YA KILOMBERO WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO
MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA WAPATIWA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO
Na: Nuru Mangalili- Ifakara TC,Habari
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Ifakara na Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba wamepatiwa Mafunzo katika kuwawezesha kutekeleza Majukumu yao kwa ufanisi na Uendeshaji wa Halmashauri zao.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa Madiwani waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025 yanalenga kuwawesha kutekeleza Majukumu yao kwa Ufanisi hususani kwenye uendeshaji wa shughuli za Maendeleo na utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Mafunzo hayo ya Siku tatu yameanza Leo tarehe 5 Januari 2026 na yanatarajiwa Kufikia tamati tarehe 7 Januari 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
Mada mbalimbali zinafundishwa katika Mafunzo hayo ikiwemo Uongozi na Utawala Bora, Sheria za Uendeshaji wa Shughuli za Serikali za Mitaa, Muundo , Majukumu na Madaraka ya Serikali za Mitaa, Uendeshaji wa Vikao na Mikutano katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Mipango Bajeti na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo, Usimamizi na Udhibiti wa Fedha Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Usimamizi wa Ardhi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,Wajibu ,Majukumu ,Haki na Stahiki za Diwani.