MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NA WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA VIZURI MIRADI YA MAENDELEO
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amewataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa Kata Wilaya ya Kilombero kusimamia ipasavyo miradi ya Maendeleo katika maeneo yao.
Hayo ameyasema leo Ijumaa tarehe 22 Novemba , 2024 wakati akifungua Semina ya tathmini ya Utekelezaji wa Miradi ya Shirika la Plan International Ifakara kwa kipindi cha miezi sita iliyofanyika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Edgar Maranta Ifakara.
Aidha alilipongeza Shirika hilo kwa kuwashirikisha Maafisa Maendeleo ya jamii na Watendaji wa Kata katika tathmini hiyo na kuwataka wataalam hao kuongeza ubunifu na ufuatiliaji.
" Maafisa Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa Kata, Mradi wowote unaofika katika maeneo yenu ule ni mradi wenu , nyie ni chumvi na sukari ya Maendeleo kwenye maeneo yenu, hakuna mradi wowote unaokuja ambao haukuhusu hivyo mkafanye tathmini ya uhakika". Alisema Mhe. Kyobya.






