MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yamefanyika kiwilaya katika Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo wanawake kutoka sehemu mbali mbali wamejitokeza katika kufanikisha shughuli hiyo.
Aidha wameiomba serikali kuwapatia tenda ya kuandaa shughuli mbalimbali kupitia miradi ya serikali pia kuwapatia elimu ya Ushirika na mitaji ya kuanzisha Miradi mbalimbali ya ujasiliamali ili waweze kuinuka kiuchumi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Danstan Kyobya amewasisitiza wanawake wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuwa mfano wa kuigwa Kwa kufanya shughuli zao kwa kujitegemea pamoja na kusimamia suala la maadili Kwa kupinga ukatili na vitendo visivyo faa Kwa jamii.
KAULI MBIU:
"Wekeza Kwa Wanawake; Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii."





