• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

KV -HELP YAGAWA KUKU 100 KWA WALENGWA WA KONGA ILI KUWABORESHEA LISHE NA KIPATO

Posted on: September 22nd, 2025

KV-HELP YAGAWA KUKU 100 KWA WALENGWA WA KONGA ILI KUWABORESHEA LISHE  NA KIPATO


Katika jitihada za kuboresha lishe na kipato kwa jamii watu wa ( KONGA)Wamekuwa wanufaika wa awamu ya kwanza kutoka  Shirika la Kilombero Valley Health and Livelihood Promotion (KV-HELP) limegawa kuku 100 kwa walengwa   20 wanaohudhuria kliniki ya magonjwa sugu katika Halmashauri ya Mji Ifakara kupitia Mradi wa Health Chicken unaotekelezwa na Shirika la KV- HELP , Halmashauri ya Mji Ifakara na Chuo Kikuu cha Tiba cha Mtakatifu  Francis ( SFUCHAS) ,ikiwa ni sehemu ya kuboresha maisha na lishe kwa walengwa hao.


Tukio hilo limefanyika tarehe 22 Septemba 2025 katika Ofisi za Shirika hilo lililopo Kapolo Ifakara.


Mgeni Rasmi katika tukio hilo alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Bw. Saidi Majaliwa, ambaye alipongeza hatua hiyo kama mfano bora wa ushirikiano kati ya serikali na taasisi zisizo za kiserikali katika kuinua maisha ya wananchi.




“Tunaishukuru KV-HELP kwa kuwa karibu na jamii, na kwa kuona mbali kwa kutoa msaada unaokwenda zaidi ya matibabu. Kuku hawa wanaweza kubadili maisha ya walengwa Hawa kwa kuwapatia lishe bora na fursa ya kujiongezea kipato,” alisema Bw. Majaliwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa KV-HELP, Bw. Iddy Mayumana, alisema kuwa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa shirika kusaidia walengwa wanaoishi na magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, na VVU  kwa njia endelevu.


“Watu wengi wanaoishi na magonjwa ya muda mrefu hukumbwa na changamoto ya lishe duni na hali ngumu ya kiuchumi. Tunatumia mbinu kama ufugaji wa kuku kuwasaidia kujenga uwezo wa kujitegemea,” alieleza Bw. Mayumana.


Walengwa waliopokea kuku hao walielezea furaha yao na kuahidi kutumia vizuri fursa hiyo. Wengi walisema kuwa msaada huo ni mwanzo wa kujikomboa kiuchumi na kuboresha afya zao kwa kula lishe bora inayopatikana kutoka kwa kuku, ikiwemo mayai na nyama.


Kwa mujibu wa KV-HELP, zoezi hilo ni sehemu ya mpango mpana wa shirika hilo wa kuimarisha afya na maisha ya watu walioko katika mazingira hatarishi kupitia miradi ya kijamii inayochangia afya na uchumi wa familia.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani