Kikao cha kamati ya lishe robo ya kwanza.
Kikao cha Kamati ya Lishe kwa Robo ya kwanza kimefanyika Leo tarehe 28 Oktoba 2024 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero.
Pamoja na mambo mengine, Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha hali ya Lishe mashuleni na pia kuzidi kutoa Elimu kwa Wanajamii juu ya Suala Zima la Lishe.




