KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
KATIBU WA CCM WILAYA YA KILOMBERO AMEWATAKA WAHESHIMIWA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINASHUGHULIKIWA KATIKA MAENEO YAO
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kilombero Ndugu Gervas Ndaki amewataka Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuhakikisha wanawajibika Ipasavyo kwenye nafasi zao kwa kuhakikisha wanatatua Kero na shida za wananchi.
Hayo ameyasema leo Disemba 4,2025 wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo aliwataka Waheshimiwa hao kuishi viapo walivyoapa na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa wananchi.
"Tuhakikishe Haki ya Mtu inapatikana asiye na haki aambiwe wewe ndio jicho , wewe ndio Mwakilishi mwende mkashughulikie shida za Wananchi katika maeneo yenu".Alisema Ndugu Gervas Ndaki