KAMATI YA SIASA IMEFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
Kamati ya Siasa ya Halmashauri ya Mji Ifakara Septemba 6,2024 imefanya Ziara na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo kwenye halmashauri ya Mji Ifakara.
Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Mohammed Msuya
Aidha, Kamati hiyo ilitembelea miradi ya Kituo cha Afya Msolwa, Shule Mpya ya Sekondari Katurukila, Shule Mpya ya Fundi Mpanga iliyopo Kata ya Kisawasawa , Hospitali ya Halmashauri iliyopo Kata ya Kiberege ,Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji Ifakara ,Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi pamoja na nyumba za Wakuu wa Idara.





