• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

HALMASHAURI YA MJI IFAKARA IMEPOKEA TAARIFA YA MRADI WA KAZIAFYA KUTOKA TAASISI YA AFYA IFAKARA (IHI)

Posted on: January 30th, 2025

Mradi huo ulitekelezwa  katika Shule nne za Halmashauri ya Mji Ifakara ambazo ni Miembeni, Katindiuka , Kining'ina na Kibaoni ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2018 hadi 2022 na Taasisi ya Afya Ifakara -( IHI)  kwa kushirikiana na Wafadhili kutoka Uswizi ( Swiss Tropical and Public Health Institute).



Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo Jumatano tarehe 29 /1/2025 , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Dkt. Yuda Mgeni aliipongeza Taasisi hiyo kwa taarifa hiyo  kwani itasaidia  jamii  katika kuhakikisha watoto wanakua katika Mazingira mazuri ya kusoma na afya bora .


" Niwapongeze kwa kazi nzuri ya utafiti ambapo matokeo utafiti huu yatasaidia Halmashauri katika kuboresha elimu na ufaulu mashuleni kwa kuhimiza mazoezi kwa wanafunzi na kuhimiza wazazi kuhusu umuhimu wa  chakula kwa wanafunzi mashuleni ". Alisema Dkt. Yuda


Aidha , Mradi huo ulitekelezwa katika nchi tatu za  Afrika Kusini, Ivory Cost na Tanzania - Wilaya ya Kilombero lengo ikiwa ni kuchunguza umuhimu wa Mazoezi ya Viungo na Virutubisho vya ziada katika ukuaji na Maendeleo ya watoto walioko mashuleni .


Mmoja wa Wanasayansi Watafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bi. Eliahika Minja alisema katika Utafiti huo walibaini mambo mbalimbali ikiwemo watoto wengi kutokupata mlo kamili kwa kuzingatia makundi ya chakula au kupata mlo mmoja hali inayochangia udumavu na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri au kushindwa kushiriki Michezo au mazoezi ya viungo, hivyo alisisitiza Elimu izidi kutolewa kwa  jamii kuzingatia kuwapa watoto chakula hasa kwa makundi yote ya chakula ili kuongeza uwezo wa kusoma  wawapo mashuleni na kusisitiza vipindi vya michezo vihusishe wanafunzi kufanya mazoezi na kucheza Michezo mbalimbali.


Mradi huu ulihusisha jumla ya wanafunzi 1,055 kutoka shule hizo ambapo wasichana 543 na wavulana 494 .

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani