"FANYENI KAZI KULINGANA NA MIKATABA YENU."TD ZAHARA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahara Michuzi amewataka Mafundi wanaofanya kazi katika Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Ifakara kufanya Kazi hizo kwa kufuata utaratibu wa Mikataba ya makubaliano ya kazi.
Hayo ameyasema Jumatano tarehe 11 Septemba ,2024 wakati alipofanya Kikao na Umoja wa Mafundi wa Halmashauri ya Mji Ifakara ( UMMI) kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
"Fuateni utaratibu na tekelezeni yaliyoko kwenye Mkataba ,msifuate maelekezo ya mdomo". Alisema Bi. Zahara
Nae Mwenyekiti wa Umoja huo Bw. Edwin Mpiwa alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia ubora, weledi na kwa wakati .




