DIWANI NDUMBA AWAPATIA ZAWADI WANAWAKE WA KATA YA MANG'ULA
Diwani wa Kata ya Mang'ula Mhe. Flora Ndumba amewapatia zawadi ya khanga Wanawake wa Kata ya Mang'ula kwenye Kikao cha Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Halmashauri ya Mji Ifakara lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ifakara ( FDC Ifakara).
Aidha Diwani huyo aliwahimiza Wanawake hao kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura tarehe 11 Oktoba hadi tarehe 20 Oktoba 2024 . Na pia kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi watakao leta Maendeleo katika Jamii.


