DC KYOBYA NA MENEJIMENTI (CMT) YA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA WATEMBELEA MASOKO YA WAFANYA BIASHARA WA SAMAKI WALIOPO STENDI YA KIBAONI NA SOKO LA KARIAKOO KATIKA KATA YA VIWANJA SITINI
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya na Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Ifakara ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Dkt. Yuda Mgeni Julai 9 , 2025 wametembelea Masoko ya Wafanyabiashara na Samaki katika Halmashauri ya Mji Ifakara katika Eneo la Stendi ya Kibaoni na Soko la Kariakoo lililopo Mtaa wa Mhola Kata ya Viwanja Sitini.
Aidha Wafanyabiashara hao walipata nafasi ya kuelezea kero na changamoto wanazokutana nazo katika Masoko hayo ambayo huanza kazi kila siku saa 9 Alasiri mpaka saa 2 Usiku.
Mkuu wa Wilaya , Kaimu Mkurugenzi na Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Ifakara walizipokea changamoto hizo na kuzifanyia kazi.
