DC KILOMBERO ATOA VYETI VYA UKAMILISHAJI WA MIRADI YA JAMII ILIYOTEKELEZWA NA WALENGWA WA TASAF 2023/2024
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya akitoa Vyeti vya ukamilishaji wa Miradi ya Jamii iliyotekelezwa na Walengwa wa TASAF mwaka 2023/2024.
Vyeti hivyo vilitolewa kwa Vijiji vya Kilama na Kibaoni ambao walitekeleza miradi ya Ujenzi wa barabara za Jamii na Vijiji vya Kikwawila na Lugongole ambao walitekeleza miradi ya Upandaji miti.
Aidha miradi hiyo yote ilifadhiliwa na TASAF
Tukio hili limefanyika wakati wa Uzinduzi wa Semina ya Mikopo ya Asilimia 10 kwa wananchi wa Ifakara iliyofanyika shule ya Msingi Kapolo.