DAS MWAIKWILA APONGEZA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero Abraham Mwaikwila, ametembelea baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari leo Januari 8,2023.
Katika matembezi hayo ameambatana na Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari ili kuangalia mahudhurio ya Wanafunzi ya uandikishaji wa Darasa la Awali na Darasa la Kwanza pamoja na uhudhuruaji wa Wanafunzi wa Kidato cha kwanza.
Hata hivyo ametoa pongezi kwa wazazi waliowaandikisha na kuhakikisha Wanafunzi wanafika shuleni na kuanza masomo yao leo .
"Hongereni sana wazazi,walimu na Wanafunzi kwa kuhakikisha masomo yanaanza leo na nitoe wito kwa Wanafunzi ambao hawajafika wajitahidi wafike ndani ya wiki hii" DAS Mwaikwila
Pamoja na hayo amewataka walimu kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kulea Wanafunzi kwa Misingi na maadili mema.

