• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA

Posted on: October 6th, 2025

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO KATIKA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA

Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo  (SUA) kimetambulisha Rasmi Mradi wa TAGDev 2.0 AGRIFOSE -RIH, unaotekelezwa chini ya RUFORUM kwa ufadhili wa Mastercard Foundation kwa Vikundi 18 vya Vijana katika Halmashauri ya Mji Ifakara, Mkoani Morogoro.

Utambulisho huo umefanyika Leo Jumatatu Oktoba 6.2025 umehusisha Vikundi vya Vijana kutoka Kata nne za Kiberege, Katindiuka, Kisawasawa na Signal ambapo Mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji na Mnyororo wa thamani wa mazao ya Mpunga na mbogamboga ukiwapa kipaumbele Vijana wakike wanaounda zaidi ya asilimia 70 ya Walengwa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo , Mratibu wa Mradi kutoka SUA , Dkt. Hamisi Tindwa alisema Mradi huo utawajengea Vijana uwezo wa kuendesha biashara katika Sekta ya Kilimo badala ya kubaki katika uzalishaji pekee.

"Mradi huu utamwezesha Kijana sio tu kuzalisha , bali pia kuchakata mazao na kushiriki katika biashara. Baada ya miaka mitano ya utekelezaji wake, kuanzia Januari 2025 hadi Desemba 2029 tutapima mafanikio kwa idadi ya biashara mpya zitakazozaliwa kupitia Vijana hawa ". AlisemA Dkt. Tindwa

kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika warsha hiyo aliwapongeza Vijana waliochaguliwa kushiriki  katika Mafunzo  hayo, akiwataka kutumia maarifa watakayopata kuongeza ubunifu, matumizi ya teknolojia na masoko ya bidhaa zao.

"Nataraji kuona Vijana hawa wakibadilika na kutumia teknolojia za Kisasa katika uzalishaji na biashara ya mazao yao. Huu ni mwanzao wa mabadiliko makubwa katika uchumi wa Vijana wetu" . alisema Mhe. Kyobya

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa aliishukuru SUA kupitia Mradi wa RUFORUM kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha Vijana katika Sekta ya Kilimo, akibainisha kuwa elimu hiyo italeta tija kubwa kwa jamii.

Mmoja wa Wasiriki wa Mafunzo hayo , Bi. Consolata Fabian kutoka Kikundi cha Promise cha Kisawasawa , alitoa shukrani kwa SUA kwa ujuo wa Mradi huo, akisema utawasaidia kupata maarifa mapya na kuongeza kipato kupitia shughuli za Kilimo Biashara.

Mradi wa TAGDev 2.0 AGRIFOSE -RIH ni sehemu ya Programu ya RUFORUM inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Chuo cha Nelson Mandela (ARUSHA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaama (UDSM), na Jukwaa la Vyuo Vikuu Afrika (RUFORUM) kwa ufadhili wa Mastercard Foundation.


Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani