• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

BODI YA PAMBA TANZANIA YAFANYA UWEKEZAJI KWA KUKODI ENEO LA KIJIJI CHA KIKWAWILA LENYE UKUBWA WA EKARI ELFU 11,000 KWAAJILI YA KILIMO CHA DENGU

Posted on: July 20th, 2025

BODI YA  PAMBA  TANZANIA YAFANYA UWEKEZAJI  ENEO LA KIJIJI CHA KIKWAWILA LENYE UKUBWA WA EKARI ELFU 11,000 KWAAJILI YA KILIMO CHA DENGU

Bodi ya Pamba Tanzania imefanya Uwekezaji wa Kilimo cha zao la Dengu  katika Eneo la Shamba la Kijiji cha Kikwawila , Muomakila lililopo Kata ya Kibaoni kwa kipindi cha Miezi Minne kuanzia Mwezi Agosti hadi Novemba 2025 ambapo Shamba hilo huwa halitumiwi na Wanakijiji kwa muda huo huwa wameshavuna Mazao  yao ambayo ni Mpunga na kusubiri msimu mwingine wa Kilimo ambacho huanza Mwezi Novemba . Aidha Mwekezaji huyo atatumia Shamba hilo kwa Kipindi ambacho Shamba linakuwa halina shughuli zozote za kilimo kwa Wanakijiji kwa muda wa miezi 4 kwa Gharama ya Shilingi  Milioni 50,000,000 ambapo Fedha hiyo itawekwa katika akaunti ya Kijiji.


Akizungumza wakati wa Mkutano wa Wanakijiji cha Kikwawila , Viongozi wa Serikali ya Kijiji, Halmashauri , Wilaya na Wawekezaji hao tarehe 20/7/2025, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliwaeleza Wanakijiji hao kuwa mbali  na Mwekezaji huyo  kukodi Ekari hizo pia  atawalimia Wananchi Ekari Elfu 2,000 kati ya Ekari Elfu 11,000 anazozikodi na kwamba Wananchi hao Watazisimamia na kuwa mfano kwa wengine.

"Ekari Elfu 11 zitalimwa kati ya hizo Ekari  Elfu 2 zitalimwa kwaajili ya Wanakijiji kila mtu atapewa azisimamie kwenye utaratibu wa Ushirika wa Kijiji, Ekari elfu 9 zitakuwa kwaajili ya Mwekezaji ". Alisema Mhe. Malima

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa  Bodi ya Pamba Aggrey Mwanri alisema katika Uwekezaji huo Wanakijiji hao watanufaika ambapo Bodi ya Pamba itachangia shughuli za kimaendeleo kwa Kijamii kama ELIMU , Afya , Miundo Mbinu n.k

Mmoja wa Wananchi wa Kijiji hicho Bw. Martine Ngwega alieleza ujio wa Mwekezaji katika Eneo hilo utanufaisha Wananchi wa Kijiji hicho kwani Kipindi ambacho wanakuwa wamevuna Mpunga eneo hilo linakuwa halitumiki hivyo kuja kwa Mwekezaji huyo kutaendelea kuongeza mapato na Ustawi wa Kijiji hicho.

"Tunashukuru Mwekezaji kwa kulichagua eneo letu, kwani pia suala la Miundombinu ameahidi kututengenezea na Vijana wetu watapata Ajira kupitia Uwekezaji huu". Alisema Bw. Ngwega


   




Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI KWA MWAKA 2026/27 HADI 20230/31
  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA, TIMU YA MENEJIMENTI WAPONGEZWA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • MHESHIMIWA KASSIM FAYA NAKAPALA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KILOMBERO AWATAKA MADIWANI KUHAKIKISHA KERO ZA WANANCHI ZINATATULIWA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani