Asanga awafuta Machozi Wahanga wa Mafuriko
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakar Asenga ametoa msaada kwa wahanga wa mafuriko leo Aprili 9,2024 katika kata ya Lipangala kambi iliyopo shule ya Msingi Kiyongwire pamoja na kata Lumemo kambi iliyopo shule ya Sekondari Mahutanga .

Jumla ya Wahanga wa mafuriko 153 wamenufaika na msaada huo ,ambapo nahitaji yaliyotolewa ni zaidi ya kilo 715 za Unga wa Sembe, mafuta ya kula Lita 160 pamoja na sukari Kg 160.
