Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Ifakara Wamesajili na Kutoa Elimu ya Mikopo ya Asilimia Kumi kwa Wajasiriamali Soko la Kariakoo Kata ya Viwanja Sitini
Posted on 06 December 2025Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Ifakara Wametoa Elimu na Kusajili wajasiriamali katika Soko la Kariakoo lililopo Kata ya Viwanja Sitini kuhusu Mikopo inayotolewa na Serikali kwaajili ya Kuwakwezesha Wananchi Kiuchumi ambayo ni Mikopo ya Asilimia Kumi inayotokana na Mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Mikopo hiyo inalenga Vikundi vya Wanawake , Vijana na Watu wenye Ulemavu (WYD) pamoja na Mikopo ya Wajasiriamali ( WBN) ambayo ni kwa Wafanyabiashara wadogowadogo wenye mtaji usiozidi Milioni 4.