• Nukuu ya Ukaribisho
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Mawasiliano Yetu
Ifakara Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Mji Ifakara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Taswira
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Biashara
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Manunuzi & Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
  • Uwekezaji
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Kapu
    • Utamaduni,Sanaa & Michezo
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos

HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YANUNUA GARI LA TAKA ILI KUWEKA MJI SAFI NA KUBORESHA MAZINGIRA

Posted on 06 December 2025

HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YANUNUA GARI KWAAJILI YA KUZOA TAKA NA KUWEKA MJI SAFI

Halmashauri ya Mji Ifakara imenunua Gari kwaajili ya kubeba taka na kuweka Mji Safi. Gari hilo limezinduliwa  Jumatatu tarehe 22 Septemba 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya nje ya Ofisi za Halmashauri ya Mji Ifakara.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana alieleza kuwa Gari hilo limenunuliwa kutokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri  na Bajeti hiyo ilipangwa ili kuondokana na adha iliyokuwepo awali ya uzoaji taka.

Wakati huohuo Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Rashidi Semngoya alisema kuwa kutokana na ujio wa gari hilo lenye uwezo wa kubeba taka  nyingi kwa wakati mmoja  alitoa wito kwa wananchi wa Ifakara kuhifadhi taka kwenye vyombo mahususi ili taka hizo ziweze kuchukuliwa kirahisis na watoe ada /tozo za taka bila shuruti.

" Ninaamini Gari hili tutalitumia na kulitunza vizuri ili liweze kutoa huduma kwa kipindi kirefu zaidi na kuhakikisha Mji wetu unakua safi muda wote ". Alisisitiza Bwana Semngoya.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka ngumu Bw. Gabriel Malisa  alieleza jinsi Mji utakavyokuwa Msafi kwani hii ni nyenzo muhimu na wananchi wanapaswa kuchangia kulipa ada za taka ili huduma hiyo iendelee kuwa nzuri.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi wakati wa Hafla hiyo ya Uzinduzi Mhe. Wakili Dunstan Kyobya alisisitiza kuendelea kutolewa kwa Elimu ya Usafi wa Mazingira kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara  katika ngazi za Mtaa, Vijiji, Vitongoji, na Taasisi zote.

" Changamoto ya Usafi wa Mji ilikuwa kubwa sana , uwepo wa Gari hiii utakuwa Muarobaini wa kwenda kuondoa uchafu wote katika maeneo yote na kila Duka liwe na chomboo cha kuhifadhia taka ". Alisema Mhe. Kyobya.



Latest Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MPIGA KURA KUPIGA KURA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KITUO TOFAUTI NA KITUO ALICHOJIANDIKISHA

    read more
  • TANGAZO LA ULIPAJI WA ADA NA USHURU KWA WANANCHI, WAFANYABIASHARA NA TAASISI MBALIMBALI IFAKARA MJI

    read more
  • View More

Habari Mpya

  • BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI NA MEZA 100 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
  • CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO - HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
  • KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI . PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
  • WAZEE WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NCHINI
  • WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
  • More

Mawasiliano Yetu

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Ifakara
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Simu ya Mkononi: -

Kurasa za Haraka

  • CHF
  • Ramani ya halmashauri ya mji wa Ifakara
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2024
  • BOFYA HAPA KUOMBA KITAMBULISHO CHA WAJASILIAMALI WADOGO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2024

Kurasa Mfanano

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya utumishi wa uma
  • Tovuti ya mkoa wa Morogoro
  • Tovuti ya Ajira Tanzania

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya Uhifadhi
  • Maswali ya mara kwa mara
  • Ramani