1.Jaza ya Fomu ya Maombi inayopatkana katika Tovuti hii Sehemu ya Nyaraka
2.Ambatanisha Picha ndogo 6 za rangi pamoja na Uthibitisho wa Uraia ( Nakala ya Cheti cha kuzaliwa,nakala ya kitambulisho cha Utaifa,Hati ya kusafiria au Hati ya kiapo cha kuzaliwa kutoka Mahakamani au kwa Wakili)
3.Wasilisha Fomu yako Ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Ardhi
4.Wataalamu wa Ardhi watafanya ukaguzi wa eneo hilo ikiwa limeripotiwa kuwa na Mgogoro
5.Utapaswa kulipia gharama za maandalizi kulingana na ukubwa wa eneo husika na matumizi yake (Gharama zote zitalipwa Benki)
6.Baada ya Nyaraka kuandaliwa Mmiliki atapaswa kurudi Ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kusaini baada ya siku tatu(3)
7.Baada ya Miezi mitatu (3) Hati ya Mmmiliki itakuwa tayari
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa