PIKIPIKI 9 ZAGAWIWA KWA WARATIBU ELIMU KATA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji ifakara ndugu Francis Ndulane amewataka waratibu Elimu kata kutumia pikipiki hizo kwa shughuli za kiofisi nasio shughulizao binafsi ilikuboresha shughuli za Elimu.
Ameyasema hayo wakati wa ugawaji wa pikipiki hizo uliofanyika katika eneo la ofisi kuu ya Halmashauri ya mji Ifakara.
Hata hivyo amesema kuwa Halmashauri ya Mji imepewa pikipiki 9 kutoka Tamisemi kupitia mradi wa KKK na kufanya usajili wa bima ambayo kila pikipiki moja imegarimu kiasi cha sh:176,000/= kwa kila pikipii Halmashauri ime kabidhi pikipiki hizo zikiwa tayari zinabima ilikuboresha mfumo wa usimamizi wa shughuli za elimu Lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa elimu.
Aidha ameongeza kuwa Waratibu kata elimu wametatuliwa changamoto kwa sasa shuguli za kielimu zitafanyika kwa ufanisi na kwa wakati kukagua shule, kufuatilia ufundishwaji, kwa wanafunzi na mambo mbalimbali yanayo husu elimu kwa ujumla wake katika shuke 39 za serikali na hata binafsi katika Halmashauri ya mji ifakara.
Naye Mwenyekiti wa waratibu Elimu kata Halmashauri ya Mji Ifakara Bi Tatu Njayaga amesema ana ishukuru Serikali kuu na Halmashauri kwa kupunguza adha ya usafiri wakati wa kutembela shule kwa kuondokana na gharama ya kukodi pikipiki kwani kazi itaenda kufanyika kwa kasi na kwamda utakao pangwa .
Kwa upande wake Bi prosister kavishe afisaTaaluma Elimusekondari amesema kuwa makabidhiano haya nimazuri na ufuatiliaji ulikuwa na tabu huko nyuma lakini kwa kupata vyombo hivi vya usafiri ume warahisishia kazi wanategemea kuona ufanisi mzuri wakazi ukiendelea hakika taaluma katika Mji wa Ifakra itapanda kwa kasi na kuhakikisha mapungufu yaliyokuwepo nyuma yana tatuliwa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa