Sisi kama serikali tunaunga mkono juhudi za wananchi kwa namna moja au nyingine ili kuhakikisha wananchi wana ondokana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya afya katika kijiji hiki nakuepuka kutembea umbali mrefu kwaajili ya kwenda kupata huduma katika kituo chetu cha afya kibaoni.
Hayo ya mesemwa na Mkuu wa wilaya ya kilombero Ndugu James Ihunyo, alipo tembelea kijiji cha lumemo kuwa katika mji wetu wa ifakara kwani kituo cha afya ni kimoja pekee na zahanati za serikali tatu pekee hazi toshelezi kwa ajili ya mahitaji ya wananchi ,sisi kama watumishi wa serikali tuna himiza maendeleo katika maeneo yetu ya kazi ambayo tuna yaongoza na kuhakikisha zile huduma za kijamii zina patikana,hivyo tuka wahimiza wananchi kuanza kujenga zahanati kwa nguvu zao wenyewe ili watakapo kuwa wamefikia hatua nzuri sasa nasisi tutoe mchango wetu wa hali na mali kuhakikisha wana malizia ujenzi huu,na kwakuwa wameonyesha juhudi sisi kama ofisi ya mkuu wa wilaya tukaona tutoe mifuko 100 ya simenti kwaajili ya kumalizia ujenzi huu kwani wananci wana uhitaji mkubwa wa huduma ya afya.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Ndugu Francis Ndulane.Amesema kuwa anampongeza mh diwani wa kata ya lumemo kwa kuonyesha juhudi za kuhamasisha wananchi ili kufanikisha ujenzi wazahanati hasa ukiangalia nikilio chetu kuwa nazahanati kwani ukizingatia mpaka sasa tuna kituo kimoja cha afya na zahanati moja pamoja na vituo binafsi,kweli huduma ilikuwa niduni naukiangalia watu wanatoka umbali mrefu kuja kutibiwa kituo cha afya kibaoni au hospitali kubwa ya santa fansis , nasasa kwa wingi huo wa wagonjwa ilikuwa nilazima tupate zahanati na dispensary, kwani tunashukuru kwa kupiga hatua hii kubwa uliyo fikia katika katayako kwani hii ni zahanati ya tatu kui hamasisha na kufikia hatua nzuri .pia sisi kama halmashauri tumesha weza kuingiza bajeti kwa miradi inayo endelea ili kuhakikisha miradi hiyo haisimami na tumetenga kiasi cha sh milioni 30, kuhakikisha tuna kamilisha ujenzi wa vituo vya afya pamoja na zahanati kwa kushirikiana na wananchi.
Kwa upande wake,Mh: Getrudi Rwakatare .amesema kuwa amefurahishwa kuona mtu mmoja anaweza kusababisha kijiji kizima kiwe nafuraha na kumpongeza mzee mkwasi kwa kuiweka lumemo kwanza, na kumpongeza mkurugenzi waHalmashauri ya Mji Ifakara kwa kuonyesha uzalendo ,na mkuu wa wilaya ya kilombero ,tunashukuru kwa juhudi zako kwani kitendo ulicho kifanya nicha kiungwana, naninaomba tushikamane kuleta maendeleo katika mji wetu ifakara na mimi kama mpenda maendeleo ninapenda kuchangia katika zahanati yetu hii matofali elfu kumi,ili kukamilisha ujenzi huu.
Naye Mh: Selemani Njahame Diwani kata ya lumemo ,Amesema kuwa zahanati hii ya lumemo tupo sisi na tuna hitaji maendeleo kwa kasi nasera ya serikali kwamba kila kijiji kiwe na zahanati na katika mchakato wa kutafuta eneo tumepata mzee amejitolea eneo kwaajili ya ujenzi na kwanamna mlivyo kuta eneo nazoezi la utekelezaji likiendelea, tunashukuru kwa viongozi kufika katika eneo hili tena kwa nia ya kuhamasisha kwa kuchangia mifuko ya simenti ili kuendelea na ujenzi huu.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha lumemo Tatu Mgenda ,Ameushuru uwongozi wa Halmashauri pamoja na ofisi ya mkuu wa wailaya pamoja na mama Getrudi kwa kuonyesha mchango mkubwa ili kuifanya lumemo kuwe na huduma za afya kwani tutakuwa hatutembei umbali mrefu kufwata huduma ya afya kwa kuwa na zahanati katika kijiji kwa kupata,zahanati kwani tulikuwa tukitembea umbali mrefu mpaka kibao usiku sanyingine nauli tunakosa na kusababisha vifo,lakini tunashukuru serikali kwa kutuunga mkono kujenga zahanati tutakuwa tunapata matibabu karibu kwani tutaokoa kizazi hiki na kizazi kijacho.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa