Wananchi na Wakazi wa Morogoro wameendelea kumiminika katika banda la Maonesho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi la Halmashauri ya Mji Ifakara na wengi wameoneshwa kushangazwa na kuvutiwa na mashine ya ajabu inayototolesha vifaranga kwa kutumia taa ya chemli inayotumia mafuta ya taa.
Akizungumza na Wananchi hao waliofika kwa nyakati tofauti katika banda hilo Mjasiriamali kutoka Kampuni ya 'Chawangula Incubators' iliyopo kata ya Mlabani katika Halmashauri ya Mji Ifakara, Atanas Chawangula ameeleza kuwa mashine hiyo ya asili ambayo hutotolesha Mayai ya kuku,bata,kanga na aina zote za ndege ni ya gharama nafuu kwani hutengenezwa kwa mbao,nyavu na mabati na hutumia chemli ya mafuta ya taa katika uendeshaji wake
Chawangula ameeleza kuwa mashine hiyo yenye uwezo wa kutotolesha vifaranga 300 na kuangua kwa 100% ikiwa Mfugaji atatimiza masharti ya uangulishaji kwa kuweka Mayai yasiyozidi siku 10 tangu kutagwa
Amesema kuwa mashine hiyo ni rahisi kutumiwa na mtu yeyote ,mahali popote na katika mazingira yeyote hususani maeneo yasiyo na umeme kutokana na mfumo wake kutumia taa ya chemli kutengeneza joto la kutotolesha vifaranga
Chawangula ameongeza kuwa mfugaji anapaswa kuweka Mayai yake yasiyozidi siku 10 tangu kutagwa na kuyapanga katika trei zilizopo ndani ya mashine hiyo na kisha kuwasha taa ya chemli iliyopo nyuma ya mashine hiyo ambayo hutumia Lita 7 za mafuta ya taa kwa kipindi chote cha siku 21 za uangulishaji na hutakiwa kutoa joto la nyuzi 37 hadi 38
Amesema mashine hizo wanazitengeneza wao wenyewe na kuuza kwa gharama isiyozidi Tsh 300,000/ kwa ile inayototolesha Mayai 300 na hutumia wiki moja kutengeneza
Naye Mwananchi Chrisant Tenga amefurahia teknolojia hiyo na kuahidi kutembelea kiwanda cha Wajasiriamali hao baada ya maonesho kuisha
Katika hatua nyingine Maafisa wa Serikali toka Halmashauri za wilaya Mafia na Mvomero wametoa mualiko kwa Mjasiriamali huyo kwenda kuwatengenezea Wafugaji wao mashine hizo na kuwapatia utaalam wa kuzitumia
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa