MILIONI MIA MOJA NA TISINI (190,000,000/=) ZATOLEWA KATIKA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA KWA AJILI YA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
Katika kipindi cha Julai -22 Juni 2020,Halmashauri imekusanya kiasi cha Tsh 1,670,228,524.94/= kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato vya ndani vya Halmashauri.Katika kipindi hicho Halmashauri imetenga kiasi cha Tsh 167,022,852.49/= ikiwa ni asilimia kumi ya makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya utoaji mikopo kwa mikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Halmashauri katika mwaka huu wa fedha 2019/2020 imefanikiwa kutoa mikopo kwa awamu mbili ,
awamu ya kwanza ilikuwa Julai –Desemba 2019 imetoa mkopo wenye thamani ya TSH 130,000,000/= Kwa vikundi 27 ikiwa ni sawa na asilimia 77.83% ya kiasi kinachohitajika kutoa mkopo.
Awamu ya pili ilikuwa ni leo tarehe 25/06/2020 kwa kipindi cha Januari – Juni 2020 ya mwaka fedha 2019/2020, jumla ya
Tsh 60,000,000/= imetolewa kwa Vikundi 12 sawa na asilimia 35.92% zaidi ya kiasi cha kilichohitajika kuvikopesha vikundi kwa marejesho ya bila riba.
Kwa ujumla Halmashauri ya mji Ifakara imefanikiwa kutoa mkopo kwa vikundi 39 wenye thamani ya Tsh 190,000,000/= kwa mwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 ambayo ni sawa na asilimia 11.4% zaidi ya asilimia kumi inayohitajika kukopesha vikundi.
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa