Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametakiwa kutumia fursa kwa kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni ya huduma ya uchunguzi wa afya ya (FURAHA YANGU KUPIMA KUJITAMBU ISHI) kwani kujua Afya ni jambo muhimu na husaidia kupunguza maambukizi mapya na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi kwa watakaogundulika na maambukizi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo ambaye ni mgeni lasmi wa kampeni hiyo ya FURAHA YANGU KUPIMA KUJITAMBUA ISHI, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliyofanyika katika Kata ya Kibaoni katika Viwanja vya Soko la Kata hiyo.
‘’Kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Kibaoni na Halmashauri ya Mji kwa ujumla kujua Afya zao kwani kujua Afya kunasaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako’’. Alisema Ihunyo.
Awali Dkt Happyness Ndosi ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji, alisema kuwa Kampeni hii inamuhusu kila Mtanzani ili kutambua Afya hususani Vijana kuanzia miaka 15 hadi 25, Wanawake Wajawazito na Watoto.
Ndosi ameongeza kuwa nchi ya Tanzania mwaka 2015 iliweka malengo ya kutokomeza Ugonja huo kwa 9.3% ifikapo 2020, ambapo 90% wawewamejitambua kama wanaishi na VVU na 90% wawewamepunguza makali ya VVU kwa kutumia Dawa za kufubaza Virusi hivyo. ‘’Tanzania ni nchi ambayo imeonyesha mafanikio katika kupambana na maambukizi ya VVU kwa kiasi kikubwa kwa mwaka 2017/18 kwa kupungua kwa maambukizi kutoka 7% hadi 4% ‘’. Alifafanua Ndosi
Kwa upande wake Muuguzi katika Taasisi inafsi ya Sauti Jafari Kigoda ameshukuru kwa uzinduzi wa kampeni hiyo na kueleza huduma zinazotolewa kuwa ni Upimaji wa VVU, BP,Uzito na Urefu, Salatani ya mlango wa kizazi kwa kinamama, Kifua Kikuu, Tohara pamoja na magonjwa mengine yaambukizayo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa