Halmashauri ya Mji Ifakara imezindua kampeni kabambe ya Kuhamasisha na kuandikisha Wananchi katika mfuko wa Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa,kampeni iliyolenga kufikia 50% ya kaya zitakazoandikishwa kwenye Mfuko huo kupitia nyumba kwa nyumba ifikapo Disemba 2017.
Akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya Uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya Stendi Kuu ya Mabasi Kibaoni na kuzinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mh.James Ihunyo , Meneja wa Mfuko huo katika Halmashauri ya Mji Ifakara Bibi.Mercy Minja, amesema uzinduzi huo ni mwanzo wa kukamilisha mkakati wa kuongeza asilimia ya Wanufaika wa CHF kutoka 6.8% ya sasa hadi kufikia 50% kwa kaya 24,433 zinazoishi katika Mji wa Ifakara
Bibi.Minja amesema kuwa lengo hilo linaweza kufikiwa kwani katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti pekee kaya 363 zimeandikishwa na kuongeza kuwa katika Uzinduzi huo wa Kampeni iliyofanyika Kibaoni kaya 117 zimeandikishwa papo kwa papo na kufanya Jumla ya kaya zote zilizoandikishwa kuwa 480.
Meneja huyo wa CHF ameeleza kuwa Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanikisha kuongeza idadi ya kaya kwani kaya 65 zilijiandikisha papo kwa papo na kaya 52 zililipiwa na Wadau mbalimbali waliojitokeza katika kampeni hiyo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilombero aliyechangia kaya 10, Mbunge wa Viti Maalum Mchungaji Dkt Getrude Lwakatare aliyetuma Mwakilishi alichangia kaya 30,Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Clarence Mgumba akichangia kaya 5 huku Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii katika Baraza la Halmashauri ya Mji Ifakara, Mh.Furaha Nganya akiahidi kuchangia kaya za Wazee 20 na Watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara kupitia Mkurugenzi wao wakiahidi kuchangia kaya 200
Awali akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kilombero Mh.James Ihunyo amesema kuwa kampeni hiyo ni endelevu na itaendeshwa katika Mji mzima wa Ifakara wenye kata 9 na vitongoji vyake na kuongeza kuwa Serikali imedhamiria kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi wake kwa kufanya maboresho katika kituo cha Afya Kibaoni ambacho kimekuwa kikitoa huduma bora za Afya kwa kiwango cha juu na hivyo Serikali inaendelea na mchakato wa kukipandisha hadhi kituo hicho ili iwe hospitali ya Wilaya na kuwasihi Wananchi kujiunga na mfuko huo ili waweze kuwa na uhakika wa kujipatia matibabu pindi wanapougua hata wakiwa hawana fedha,kwani kupitia mfuko huo kaya ya watu 6 hujiandikisha kwa Tsh.10,000/- tu na kupatiwa huduma za Afya kwa mwaka mzima.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa lengo la Mpango huo ni kuandikisha kila Mwananchi ifikapo 2020 ili kuwahakikishia matibabu na amewataka viongozi wote wa Serikali za Mitaa kushirikiana na Waandikishaji kupita nyumba hadi nyumba na kuhakikisha 100% ya Wananchi walioandikishwa inapatikana. kwa wananchi watakaojiandikisha.
Kwaupande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Ifakara Dkt.Happyness Ndossi amewashauri wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wingi ili kuviwezesha vituo vya Afya na Zahanati kununua dawa nyigi na kuweza kuwahudumia Wagonjwa wote walio katika Mfuko wa CHF kwani kadiri wanavyojiandikisha wengi ndivyo Serikali pia inaongeza hela na kununua dawa nyingi zaidi zitakazotosheleza kwa Wagonjwa wote na amesisitiza kuwa Kituo cha Afya kibaoni kimejiandaa vyema na kina uwezo mkubwa wa kuwapokea na kuwatibu magonjwa mbalimbali Wagonjwa wote wanaotibiwa kwa CHF
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa