Uchaguzi uli simamiwa, na Honesta Ngolly Afisa elimu wizara ya kazi, kutoka ofisi ya kamishina mkuu ,ili kusimamia kufanya uchaguzi wa katibu na katibu msaidizi, kwa kupiga kura ya siri na badae baada ya uchaguzi, kupata katibu huku ndugu felikx mloka, akishinda kwa kura 32,na katibu msaidizi bi esther mtweve akishinda kwa kura 11, na kuanza kazi rasmi baada ya kuchaguliwa, kwani baraza hili nichombo rasmi cha mawasiliano baina yetu, sisi watumishi na baraza kama baraza litakuwa likiwapa, ushirikiano uwongozi wa juu.
Uzinduzi huo ulio fanyika, katika ukumbi wa mikutano na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Dasi Mkoa na Mkurugenzi Halmashauri ya Mji, vyama vya wafanyakazi, wawakilishi TLG, TUG,CWT pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi, katika halmashauri ya mji ifakara, ili kuweza kukaa pamoja na kujadili mambo yote yamsingi yanayo husu halmashauri ya wilaya ,kwani baraza la wafanyakazi ni chombo cha kisheria, na kimeundwa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza Afisa Tawala Mkoa ,Ndugu Clifford Tandari. Amesema kuwa, angependa kuona bajeti, inatengwa kwaajili ya kuweka taa za barabarani, kwenye maeneo yote yenye giza, ilikuepukana na vitendo vya uporaji, ubakaji,ikiwemo vitndo vya kiovu kuto tokea, pia wananchi wawe huru, na salama zaidi. ameongeza kuwa halmashauri yetu, inakadiriwa kuwa na viwanda zaidi ya [100], vya kuchakata mpunga, kwa hivyo wafanya biashara, toka sehemu mbalimbali ,wana kuwa wengi na msongamano unakuwa mwingi.
Kwa hivyo watu waogope vidole, kuepukana na gonjwa balaa la maambukizi ya, virusi vya ukimwi, kwani wilaya na mji wa ifakara, mnaongoza kwa maambukizi ya ukimwi kwa asilimia8.7, kwaajili ya uwingi wa watu, wanao kuja kufanya biashara hapa, wananchi myaepuke haya, ilikupunguza ongezeko kubwa la maambukizi kwa kutumia kinga.
Naye mkurugenzi wa mji wa Ifakara Ndugu Farancis Ndolene, alimhakishia katibu tawala wa mkoa wa Morogoro kuwa swala la kuweka taa za barabarani, atalifanyia kazi kwa kuweza kulipangia bajeti ili kuweza kutekelezwa, kwa malengo ya kuepukana na vitendo viovu ambavyo vinaweza kuleta athari kwa siku za usoni.
Hata hivyo swala la kuweza kupambana na swala la kuepukana na virusi vya UKIMWI litafanyiwa kazi ilikuweza kupunguza maambukizi ya ukimwi kufuatia watu kuepukana na balaa la kuambukizwa kupitia nia za mbalimbali kupitia idara ya maendeleo ya jamii, kuepuka swala la vidole, na kumbi za starehe kwa watu wanaokesha zinaweza kuwa chachu ya kuchochea maambukizi ya virusi vya UKIMWI vikapungua.
Kwa upandewake Ndugu Felix Mloka .Amesema kuwa, anawashukuru wafanyakazi wenzake, kwa kumchagua kuwa katibu wa barazala la wafanyakazi, kwani kimsingi baraza hili, nichombo cha mawasiliano cha kumshauri Mkurugenzi, na nitahakikisha nawatendea haki wafanyakazi , kwa kupitia kanuni na sheria kama ilivyo sainiwa na kamishina wa kazi kwenye maelekezo yake, ntajitahidi kuitisha vikao vya baraza mapema, kwa mujibu wa taratibu zilizo wekwa, kwa kuandaa mapema vikao, na kutatua kero zao, na kuzi wakilisha katika baraza, ilikuzifanyia kazi mapema na kuziingiza kwenye, kikao cha kawaida, ili yaweze kujadiliwa na kutatuliwa. Natukienda vizuri ndani ya miaka mitatu hii, hakuta kuwa na changamoto, kwani hili linawezekana tukiwa na ushirikiano, na ninaamini kama tumeweza kuunda baraza tuta hakikisha, kero za wafanya kazi zina kwisha kabisa,na tutatenga bajeti ya kutosha.
waliyo chaguliwa kwa ajili ya kuongoza baraza hilo walikuwa ni Falix Mloka ambaye alipata kura 32 na makamu wake alikuwa ni ndugu Estha Mweve ambaye alipata kura 11, ambapo walisimamiwa na Afisa Elimu kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Ndugu Honesta Ngolly.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa