Wavuvi wa Halmashauri ya Mji Ifakara watakiwa kulinda Mto Kilombero na Mabwawa yanayopatikana katika Halmashauri yao kwa kupinga Uvuvi haramu na kutoogopa vitisho vya Wavuvi haramu hasa hasa wanaotumia Kokola yaani Nyavu inayovua Samaki Wadogo Wadogo na kuharibu Mazalia ya Samaki.
Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Lipangalala Mh.William Makoti Alipokua anafungua mkutano wa wavuvi uliyofanyika Kivukoni katika siku ya Wavuvi Duniani ambayo uadhimishwa tarehe 21 mwezi wa 11 kila mwaka .
‘’Ulinzi wa kokola ni sisi wenyewe na tukisema hatutaki uvuvi haramu kutoka moyoni basi uvuvi haramu hautokuwepo, kwani wao ni wachache kuliko sisi na sheria inaturuhusu kulinda mito na mabwa yetu cha muhimu tushirikiane kulipinga jambo hili ili vizazi vyetu vije kunufaika na mto huu’’. Alisisitiza Makoti.
Kwa upande wake Ndg.Masamja Joram ambaye ni Afisa Uvuvi Halmashauri ya Mji Ifakara alianza kwa kufafanua vifungu vya sheria za Uvuvi na kanuni zake ambazo zinatoa muongozo wa namna ambavyo Jamii itahusika katika kusimamia Rasilimali za uvuvi.
‘’Sera ya Uvuvi ya mwaka 1997 inaelekeza namna ambavyo Rasilimali za Uvuvi zinatakiwa zisimamiwe na jamii husika halkazalika sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 inaelekeza pia namna ambavyo Jamii itahusika katika usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, na kanuni za mwaka 2009 pia ivyo ivyo zinatoa muongozo wa Jamii kuhusika’’. Alifafanua Masanja.
Baada ya ufafanuzi huo Masanja aliwataka Wavuvi hao kushirikiana na uongozi wa Kata kuunda Jumuiya Shirikishi ya Wavuvi yaani BMU (Beach Management Unit) kama inavyoelekezwa na sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003 kuwa jamii husika isimamie na kulinda Rasilimali za Uvuvi ili kutokomeza Uvuvi haramu.
Kwa upande wa Wavuvi wamekubali jambo hilo na kupanga tarehe ya mwisho wa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uwongozi wa jumuia hiyo ambayo ni tarehe 10/01/2019 na uchaguzi utafanyika tarehe 20/01/2019.
Jukumu la kulinda Rasilimali za Taifa ni la kila Mtanzania hivyo utakapoona uharibifu wa Rasilimali yoyote. Tafadhari toa taarifa kwenye vyombo vya sheria ili kuinusuru Rasilimali hiyo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa