MKURUGENZI AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA KUHUSU KUVUNJWA KWA SOKO
Mkurugenzi wa Halmashauri na jopo lake la wataalamu kutoka halmashauri, mwenyekiti wa soko (UWASOKI) pamoja na wafanya biashara wote wa soko la Ifakara mjini wamefanya usafi wa mwisho wa mwezi katika soko hilo ili kuweka mji katika hali ya usafi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ndugu Francis Ndulane amezungumza na wafanya biashara hao mara baada ya kumaliza kufanya usafi na kuwatoa hofu juu ya kuvunjwa kwa soko hilo ,kwani amesema soko litavunjwa mara tu watakapopata fedha za kuendeleza zoezi hilo la kujenga soko la kisasa kwani bado wapo kwenye mikakati huku tukiwatengea maaneo maalumu ya kuwahamisha kwa muda wakati ujenzi huo ukiendelea.
Hata hinyo Ndulane amsema kuwa Kwa walio wengi wamelipa kodi vizuri na kwa wakati lakini pia wametunza mazingira vizuri na kawaasa waendelee kuboresha mazingira ili kuleta maendeleo katika Halmashauri yetu.
Ndugu Ndulane pia kasema watafanya maboresho kwa kuanza na miundo mbinu ya soko kwenye upande wa choo kwani choo ni cha zamani sana pia kwa mwaka unaoisha huu 2017/18 wamekusanya jumla ya shiligi Bilioni 2 na milioni 3 sawa na asilimia 53.7 ya makadirio ya Bilioni 3.17. Pia alisema wame kubaliana na watu wa sokoni kutozwa ushuru kutokana na vizimba kwa kodi ya kiasi cha sh. 70,000/= ili wafanye biashara kwa faida , lakini bado kuna kodi na ada ya uzoaji wa taka kupitis sheria ndogo ambazo tunazitumia kwa sasa.
Kwa upande wake Ndugu Hamis Ruvu mwenyekiti wa soko kuu la ifakara (UWASOKI) ameshukuru uongonzi wa Halmashauri kwa kuwapa kipaumbele na kuwashirikisha kila hatua wanayopiga kimaendeleo na kuishukuru Halmashauriya Mji kwa kuboresha miundombinu ya taka kwa kununua vifaa na kupunguza changamoto ya mlundikano wa taka.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa