Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mh. Ismail Mlawa pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara ndugu, Kanyala M. Mahinda leo tarehe 17/7/2020 walitembelea Kituo cha afya Kibaoni kwa lengo la kuwatambua watumishi wa Kituo hicho. Pamoja na mambo mengine, wamesisitiza juu ya kufanya kazi kwa bidii, pamoja na ushirikiano wa kila idara ili kuleta chachu ya mafanikio katika kituo hicho. Aidha, Mkurugenzi wa Mji ifakara ameahidi kufuatilia kwa ukaribu mchakato wa kupandisha hadhi ya Kituo hicho cha Afya kuwa Hospitali.
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa