Zaidi ya mifuko mia moja [100] ya simenti imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ilikufanya uhamasishaji wa ujenzi wa zahanati, pamoja na kituo cha afya katika kijiji cha lumemo, ilikupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya kibaoni, kwa kuhamasisha wananchi kuanza kujenga vituo vya afya na zahanati, kwa ajilili ya kupanua huduma hizi.
Akizungumza jana Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Ndugu James Ihunyo alipo tembele wogonjwa na kuwafariji pamoja na kuwapa zawadi ya heri ya mwakampya katika hospitali ya kibaoni katika mjiwetu wa ifakara kwa lengo la kuwapa pole.Amesema kuwa kutokana na changamoto waliyo kutana nayo,katika kituo hicho niupungufu kwenye hodi ya kinamama na watoto, kwa kuliona hilo wametaka kupanua chumba hicho cha leba na kuongeza vitanda,ilikupunguza mrundikano na wazazi kulala kitanda kimoja zaidi ya wagonjwa wawili pamoja na watoto wao katika kitanda kimoja.
''Aidha Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Ifakara Ndugu Francis Ndulane, amesema kuwa kwa mwaka 2018/19 wamatenga kiasi cha shilingi milioni stini [60] ilikusapoti ujenzi wa zahanati pamoja na vituo vya afya, katika mjiwetu wa ifakara na kutokana na uhamasishaji ambao tayari umesha fanyika, kuna zahanati katika kijiji cha Ihanga, kijiji cha Mahutanga, amba vyo tayari vimefikia hatua ya boma. pamoja na kijiji cha lumemo, ambapo wamesha tenga maeneo mawili kwa ajili ya zahanati, pamoja na kituo cha afya. pia tuta peleka mifuko mia [100], kwaaji ya kusapoti ujenzi huo. katika kijiji cha kilama , tuta peleka mifuko mia ilikukamilisha zahanati hizo. ilikupunguza msongamano wawagonjwa, katika kituo chetu cha afya kibaoni . kwa wale wagonjwa wanao toka sehemu mbalimbali za mji katiaka mkoa kilombero, kwa ajili ya kufuata huduma nzuri inayo tolewa hapa.''
Pamoja na hayo, kwanza tume kuja kuwafariji wagonjwa na kuwatakia heri ya mwaka mpya, wajiandae sasa kujiunga kwenye mfuko wa bima ya afya yaani CHF iliyo boreshwa , kwani tumeona namna tunavyo nufaika nayo , kwa kaya moja yenye watu sita wanaweza wakatibiwa kwa garama ya shilingi elfukumi [10000], kwa mwaka mzima .na kwakuwa tayari tumesha anza mchakato wa kila kata kuwa na kituo cha Afya ,kwahivyo tunaamini wakiwa kwenye fursa ya kujiunga na mfuko wa CHF iliyo boreshwa , wanaweza wakawa wanaji hakikishia, kuwa na afya bora. natunaamini hivyo kwani vituo, binafsi pamoja na taasisi binafsi ,tumesha ingianazo mkataba kwa ajili ya watumiaji wa CHF iliyo boreshwa. ilikupata huduma katika vituo hivyo. Amesema Mh. Mashaka Mbilinyi, Mwenyekiti Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kwa upande wao wagonjwa walio kuwepo siku hiyo hospitalini hapo , wameupongeza uwongozi wa Wilaya na Halmashauri ,kwa kuja kuwajulia hali na kuwafariji , na kusema kuwa wamefurahishwa na huduma ya kituo hichi cha afya, kwani wanapokea wagonjwa vizuri, kwa kauli nzuri, ukizingatia tunazipata sifa za hospitali hii na ndomana tuna kuja kutibiwa hapa ,kwani wa hudumu wa hapa wana kauli nzuri ,wagonjwa tuna patiwa huduma kwa wakati ,na dawa zinapatikana kwa wakati, ukizingatia tumetoka mbali.
Naye mganga mfawidhi Dk Joyce Mbata . Amesema moja ya changamoto tunayo kutana nayo, kwani tunapokea wagonjwa wengi kutoka wilaya tofauti tofauti kwa 70% , kama Halmashauri ya Wilaya Ulanga ,kiberege na mangula kwani tunafanya kazi ya kuhudumia, halmashauri nyingi kwahivyo tuna kuwa nachangamoto ya kuwa na wauguzi wa chache, kulingana na wagonjwa, tunao wapata . kwani tunaiyomba serikali, ipandishe hadhi kituo chetu cha afya, ilituweze kupata wa hudumu wa kutosha, na tufanye kazi kwa bidii na kwa wiledi zaidi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa