Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Ifakara Ndugu Francis Ndulane ,amekubali kuwa baba mlezi wa kituo cha Ebeneza ,amesema kuwa atahakikisha ana hamasisha wadau mbalimbali, kusapoti watoto hawa ,ilikuweza kuendeleza kituo hicho na vijana walioko hapa ili kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya maisha ya baadae, kielimu kwa namna moja au nyingine.
Mkurugenzi ameyasema hayo, alipotembelea leo kituo hicho kilichopo Ifakara mjini, kwa lengo la kutatua changamoto, zinazo wakabili watoto hao nakutoa viti arobaini (40) pamoja na meza kumi (10), kwa ajili ya kupunguza changamoto mojawapo, wanayo kutana nayo vijana hao. katika kituo chao bila kusahau kuwa afya ya vijana hao niyamuhimu zaidi akaona nivyema kuwapatia na kadi za CHF iliyoboreshwa, kwa kila kijana aliyeko kituoni hapo, ilikuepukana na gharama za matibabu pamoja na kuboresha afya zao.
Kwa upande wake mama mlezi wa kituo hicho, Bi Tekla . ameupongeza uwongozi mzima wa Halmashauri kwa kuonyesha moyo wa dhati, na wakujitolea kutaka kusaidia vijana hawa na kumuomba Mkurugenzi wa Halmashauri kuwa baba mlezi, kwani walisha ondokewa na baba mlezi miaka iliyopita kwani wamefurahi kwa kupata mlezi tena
''Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Ifakara Mh. Mashaka Mbilinyi, amesema kuwa wanaunga mkono kwa namna moja, au nyingine, na kuanza kutatua changamoto moja baada ya nyingine, kwa kuifanya kwanza ardhi yao iongezeke, kwa kutenga bajeti inayokuja ya mradi wa kupima viwanja, kwa kiasi cha bajeti yetu sisi madiwani, tunakuomba Mkurugrnzi utushawishi katika bajeti yetu, tutenge kiasi kidogo cha fedha, kwa ajili ya watoto wetu ili tunapoishi na kuboresha huduma zetu, wakupewa kipaumbele ni watoto hawa na kuhakikisha changamoto zinapungua kwa kiasi fulani . pia amempongeza Mkurugenzi wa Mji kwa kutawazwa rasmi kuwa baba mlezi wa watoto hao, nakuonyesha kuguswa yeye kama mzazi.''
Pamoja na hayo Mh.Lijua Likali amesema kuwa anaunga mkono Halmashauri kwa kuwakumbuka watoto hao,kwani kufanya hivyo ni ibada, na kushauri kuanza na kutatua changamoto ya ukosefu wa mabweni, ili kuwatenga vijana wa kiume na wa kike, na kuahidi kwa mwaka ujao 2019 atalipia bima ya afya ya mwaka mzima kwa vijana hao.
Tunapenda kukushukuru kwa mwaliko wako pia tutaendelea kushirikiana kwa pamoja na wadau mbalimbali, kuhakikisha watoto wana kuwa katika mazingira mazuri ,na bora zaidi na kutoa ushirikiano kwa kile ambacho tutaona kinafaa kwa namna moja au nyingine, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Amesema Ndulane.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa