Afisa Elimu vifaa na takwimu Halmashauri ya Mji Ifakara Esther Kirima amewataka walimu kuonyesha ujuzi walionao kwa kushiriki ana kwanza wao kwa wao ili kuleta mabadiliko ya taaluma katika Halmashauri ya Mji Ifakara lengo ikiwa ni kutokomeza ziro na divisheni 4.
Ame yasema hayo wakati wa mafuzo kazini yanayo endelea kufanyia katika ukumbi wa shule ya Ifakara sekondari wakati wakipitia mada mbalimbali moja ikiwa ni kwajinsi gani wana weza kumuinua mtoto mwenye uwezo wa chini mpaka kufaulu.
Hata hivyo Esther Kirima amesema ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa walimu wote wanao fundisha shule katika Halmashauri ya Mji kukumbushia ujuzi kila baada ya muda flani kulingana na sayansi na teknolojia ili kuwa na namna moja ya jinsi ya ufundishaji ambazo kila mmoja ali kuwa ana namna ya tofauti ya ufundishaji ili kuondoa sifuri na divisheni 4 kuanzia kidato cha 1 mpaka 4.
Kwa upande wake Afisa Taaluma sekondari Bi Prosister kavishe amesema kuwa mafunzo haya ni kwa ajili ya walimu kufanya kazi yao kwa ufasaha kwani wana fundishwa mada mbalimbali ili kuandaa masomo yao vizuri wanapo ingia kufundisha wawe na uwelewa mkubwa zaidi ili kuendana na mfumo wa sasa wa ufundishaji na kuinua Taaluma katika Halmashauri ya Mji.
Naye mwalimu Nyerere kutoka Shule ya sekondari Mlabani mseminishaji ame ipongeza Halmashauri kwa kuona umuhimu wa walimu kubadilishana ujuzi na na mnagani bora ya kuwa fikishia ujumbe wototo katika kurahisisha kazi ya ufundishaji na kujifunza kwa wanafunzi mashuleni ili kuongeza ufaulu katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa