MAAZIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMA KATIKA MJI WA IFAKARA
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika jamiii licha ya changamoto zinazowakabili kwani serikali inafahamu na inayafanyia kazi.
Hayo yamesemwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya mji ndugu Francis Ndulane wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi ya umma nchini ambapo kila mwaka hufanyika june 16 ambapo katika mji wa Ifakara maadhimisho hayo yamefanyika Katika Ukumbi wa Machipi maeneo ya Katrini.
Maadhimisho hayo yana malengo ya kutambua mchango wa watumishi wa umma katika utoaji wa huduma kwa wateja ili kuleta maendeleo kwa mwaka huuambao yambeba ebeba kauli mbiu isemayo “kuimarisha ushirikishwaji katika utoaji wa huduma vijana washirikishe kuleta mabadilko barani afrika”.
Hata hivyo Ndulane amesema kulingana na kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya “HAPA KAZI TU” inawataka watumishi kufanya kazi kwa weledi na kujituma kuwajibika na kufuata kanuni na taratibu huku akiwataka Watumishi kutojihusisha na tabia ya ubadhirifu wa fedha na mali za Umma kwani ni kosa kisheria.
Pia amesema Mtumishi kutokuwepo kazini bila taarifa ni kosa kwa mujibu wa kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma kwani kwa kufanya hivyo hupelekea kuwakosesha Wananchi huduma Wanazozihitaji na hivyo kurudisha nyuma jitihada a kuleta maendeleo na alisisitiza Mtumishi yeyote atakaekiuta taratibu za Utumishi hatua stajhiki zitachukuliwa dhidi yake.
Pamoja na hayo amewataka watumishi kutoa ushirikiano mzuri kwa mamalaka husika inayofanya kazi ya ukaguzi wa vyeti vya watumishi ili kubaki na wafanyakazi wenye sifa stahiki na ameeleza kuwa kutokana na zoezi hilo la uhakiki wafanyakazi 22 wa halmashauri ya mji wamekumbwa na sakata la Vyeti feki , kati ya hao watumishi 14 ni wa idara ya elimu Msingi ,6 idara ya Afya Mtumishi 1 idara ya ujenzi ,1 kitengo cha manunuzi .
Kwa upande wao Watumishi wa idara mbalimabali walimshukuru Mkurugenzi kwa kazi na uongozi mzuri pamoja na hayo wamesisistiza swala zima la upandishwaji wa mishahara,na upandishwaji wa v yeo pamoja na stahili zao nyinginezo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa