Walimu Wakuu wa Shule za Msingi pamoja na Waratibu Elimu Kata wa Halmashauri ya Mji Ifakara wamepokea maagizo juu ya mpango kazi wa kukuza taaluma katika shule zote za msingi za Halmashauri.
Hayo yameelezwa na Afisa Elimu Taaluma Msingi Halmashauri ya Mji Ifakara Mwl. Joha Mlindwa ambaye aliudhulia kwenye kikao kilichofanyika Mjini Dodoma tarehe 17 na 18 mwezi wa 9 mwaka huu, Kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Mwl.Mariam Nnauye. Kikao hicho kilichoitishwa na viongozi wa Ofisi ya Raisi TAMISEMI na Wizara ya Elimu.
Mpango kazi huo umewasilishwa leo na Mwl. Joha katika mkutano uliofanyika Shule ya Msingi Mapinduzi, ambao uliwajumuisha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Waratibu Elimu Kata na Maafisa Elimu Msingi Wa Halmashauri ya Mji.
Ambapo ametaja maagizo hayo kuwa ni Kusimamia utendaji kazi wa Walimu, Ufunguzi wa shughuli ya kiserikali utakaofanyika Shuleni kuanza kwa kuimba wimbo wa taifa na wimbo wa kizalendo kwa kuzingatia mafundisho yaliyomo katika wimbo huo, Kutoa taarifa kwa wakati na kuandika katika uwandishi bora, Miradi ya maendeleo itekelezwe kwa wakati, Kamati za shule zisijihusishe na uchangishaji wa fedha za majengo ya shule, Michango ya ujenzi wa shule ichangiwe na wanajamii wote ikisimamiwa na serikali za vitongoji au Mtaa, Kuhakikisha wanafunzi wa MEMKWA wanafundishwa ipasavyo, Kudhibiti utoro na uvivu wa Walimu, Walimu kumaliza mada walizopangiwa kufundisha na kutoa mazoezi ya kutosha, Ni marufuku Mwalimu kumuita Mwanafunzi majina mabaya au ya udhalilishaji, na vyumba vya madarasa ya Awali, la kwanza na la pili viwe bora kuliko vyumba vyote.
Kwa upande wa Afisa Elimu Msingi Mwl. Mariam Nnauye amewaasa walimu hao kutekeleza maagizo hayo na kuwapongeza kwa maandalizi mazuri ya mtihani wa darasa la saba.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa