MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA JUNI 29, YENYE KAULI MBIU “MAENDELEO ENDELEVU 2030”, YAKILENGA KUIMARISHA ULINZI NA FURSA SAWA KWA WATOTO
Watoto wa Halmashauri ya Mji Ifakara wakiazimisha siku ya mtoto wa Afrika ikiwa ni kumbukumbu ya mauwaji ya watoto huko kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini yaliyotokea mwaka 1976 siku kama ya leo, ni miaka 56 tangu kushiriki kwa maadhimisho hayo kwa kuungana na umoja wa mataifa (UN).
Hayo yamesemwa na Bi. Rosemary Jacob Afisa Elimu msaidizi sekondari, wakati wa maadhimisho ya siku ya watoto wa Afrika, yenye kauli mbiu ya maendeleo endelevu 2030 kuimarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto.
Afisa huyo alisema kuwa maadhimisho haya yanalenga kumlinda na kumletea mabadiliko yakielimu mtoto dhidi ya vitendo vya kikatili vinavyoendelea katika jamii zetu za kiafrika.
Pamoja na hayo Bi. Rosemary Jacob alisema kuwa changamoto ambazo wamekutana nazo watoto wa shule za kutwa katika Halmashauri ya Mji Ifakara ni ukosefu wa chakula wakati wa mchana wakiwa shuleni hali ambayo hupelekea kushindwa kuelewa masomo vizuri.
Afisa huyo wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Rosemary ameishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa mtoto kwa kutoa zawadi kwa watoto wote walioshika nafasi ya kwanza mpaka ya nne ili iwe motisha na kuboresha nyenzo za kumnyanyua mtoto kielimu.
Maadhimisho ya mtoto wa Afrika yalifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Mlabani iliyopo katika Halmashauri ya Mji Ifakara na kushirikisha wadau mbalimbali wakimaendeleo katika Halmashauri yetu.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa