MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA ELIMU
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero ndugu Robati Selasela Ameitaka Halmashauri ya mji Ifakara Kuhakikisha inazingatia motisha kwa watumishi wanao fanya vizuri kwani sio swala la hiyari nilazima ili kuhakikisha maendelo katika elimu yanafika mbali.
Akizungumza mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyo fanyika katika shule ya msingi Lipangalala amesema kuwa licha ya kutaka mtoto kujua kusoma kuhesabu na kuandika pia Halmasahuri izingatie lishe kwa watoto shuleni huku akipinga vikali mimba kwa wanafunzi.
Hata hivyo ameipongeza Halmashauri na wadau wa maendeleo ya elimu kwa ujumla katika kushiriki kikamilifa katika kumjenga mtoto kwa kushirikiana na jamii na kufaulisha kwa wastani wa 75% kwa mwaka 2016/17.
Kwa upande wake Bi. Mariamu Nnauye Afisa elimu msingi amesema wiki hii ya elimu inazungumzia utekelezaji mpango wa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu .Halmashauri imeshirikiana na wadhibiti ubora wa Elimu ili kuhakikisha kuwa na vigezo vinavyo takiwa kutekelezwa.
Ameongeza kuwa ukuzwaji wa stadi za kufundishia umesaidia kufaulisha kutoka wastani wa 65% hadi kupanda kufikia wastani wa 75% Halmashauri ikishirikiana na waje,uwawa, waelimisha jamii kwani wote wamepata stadi za kkk.
Huku walimu wa shule zilizo fanya vizuri zikiji nyakulia zawadi vyeti pamoja na pesa taslimu katika maadhimisho hayo ambayo yana kaulimbiu isemayo ‘’UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KATIKA KUTOA ELIMU BORA’’.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa