KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2017 AWATAKA WAKAAZI IFAKARA KUCHANGAMKIA FURSA YA UCHUMI WA VIWANDA
Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametakiwa kuchangamkia fursa ya uchumi wa Viwanda kwa kulima kwa wingi zao la mpunga baada ya kufunguliwa kwa kiwanda cha kisasa cha kukoboa na kuchakata Mpunga cha Ifakara White Milling Plant chenye uwezo wa kukoboa tani 60 za mpunga sawa na magunia 600 kwa siku moja.
Hayo yamesemwa Juni 16 na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2017 ndugu Amour Hamad Amour wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika eneo la Uwekezaji wa Viwanda lililotengwa na Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo tayari kiwanda hicho cha kuchakata Mpunga kimejengwa na tayari kimeanza kufanya kazi .
Aidha ndugu Amour amesema kuwa kiwanda hicho kinalenga kuleta mabadiliko ya uchumi na kutoa ajira kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa pamoja na kuongeza mahusiano kati ya vijiji na miji na kutoa faida kubwa kwa wauzaji wa Mpunga kwani ni kiwanda kinachojali maslahi ya Wananchi.
Hata hivyo amesema juu ya uwepo wa kiwanda hicho kutatatua changamoto za miundominu ya barabara kwani wawekazaji hao wataiwezesha serikali kwenye kodi na kusonga mbele kwenye maendeleo ya Taifa hili.
Pamoja na hayo ndugu Amour amewataka wananchi wa Ifakara na Wilaya ya Kilombero kutowasikiliza baadhi ya viongozi wanaorudisha nyuma maendeleo ya taifa kwa kushinikiza wananchi kutoshiriki kwenye shughuli za maendeleo na kwa kufanya hivyo watapiga hatua zaidi kwa kubadilisha maisha yao ya kila siku.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Ifakara White Milling Plant ndugu Francis Muhuga amemshukuru Kiongozi huyo kwa kuuleta Mwenge wa Uhuru 2017 hicho na kuongeza kuwa wao kama kampuni wanaunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika azma yake ya kulifikisha taifa katika Uchumi wa viwanda.
Kiwanda cha Ifakara Rice Milling Plant kipo eneo la Katindiuka umbali wa km 4 kutoka makao Makuu ya Halmashauri ya Mji Ifakara kilikamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Tsh milioni mia mbili ishirini na mpaka sasa imetoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi 10 na vibarua wa msimu 15
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa