Mh. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Ifakara, Ndugu Chiza Hasani Shungu ,amewataka wafanya biashara wa bidhaa mbalimbali, zikiwemo za mifugo na mazao ya kilimo, pamoja na bidhaa za viwandani, wauzaji wadogo wa vyakula [mama ntilie], pamoja nawauzaji wavinywaji baridi, katika mji wetu wa ifakara. kuchanga mkia fursa ya kupata maeneo katika eneo hilo la mnada, ili iwesehemu yao ya kuuza bidhaa na kununua bidhaa, kwa lengo la kuwainua wafanya bishara hao kiuchumi.
Mh. Makamu Mwenyekiti ameyasema Hayo wakati wa uzinduzi huo wa gulio katika Halmashauri ya mji ifakara kata ya michenga ulio hudhuriwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji ifakara, wa heshimiwa madiwani ,pamoja na wataalamu wa sekta mbalimbali, pamoja na wakuu wa idara wakiwa na lengo moja lakutaka kuifanya Halmashauri yetu kuwa yenye kiwango chajuu cha maendeleo.
Leo Halmashauri imeona iweke ratiba ya kuwa na gulio, kilajumamosi ya wiki inayo anziwa na tarehe moja, nakuishia na tarehe moja, ili iwe sehemu yao ya kuuza bidhaa na kununua bidhaa , pia tuweze kutumia rasilimali zilizopo hapa, bila uharibifu wowote na kuhakikisha tunaitunza amani, katika gulio hili. kwani nichachu ya maendeleo katiaka halmashauri yetu ya mji ifakara. Amesema Mh.Shungu.
'' Aidha Mkurugenzi wa halmashauri Ndugu Francis Ndulane amewakaribisha wananchi wote katikashuhuli nzima ya uuzaji wa bidhaa, na kusema kuwa kimsingi waliona eneo hili, halitumiki ipasavyo, tangu halmashauri mama iache kufanya shughuli za minada, wakaona si vema likae bila kufanyika kwa shuguli zozote, wakona nibora kuendeleza shughuli za mnada pamoja na gulio, kwa manufaa ya Halmashauri na wafanya biashara pia.
Kwani nieneo kubwa linaulinzi wa kutosha, na lenye mahitaji ya muhimi kama choo,na kusema kuwa wenyemifugo ,wenyematunda, wenyevinywaji baridi, nyamachoma,nguo,wenye mbogamboga na bidhaa nyinginezo, zenye uhalali wakuuzwa gulioni ,ziletwe. mchanga mkie fursa ya kupata maeneo, kwa ajili ya kufanyia biashara kwani nieneo zuri, kwa kupumzika nafamilia zetu .amani ipo na usalama wakutosha. kwani shuhuli hii imebarikiwa na baraza letu la madiwani kwahiyo tuta kuwa tukiendesha shulizetu kwa utaratibu na kwa mujibu wa sheria Amesema Ndulane.
Kwa upande wake Mh.Joakim Luselo diwani kata ya michenga ameupongeza uwongozi wa Halmashauri kwa kuona shuguli za mnada zikiendelea katika eneo lake na kuahidi kusimamia vizuri shughuli zitakazo endelea katika eneo hilo kwa kufuata taratibu na sheria zilizo wekwa na Halmashauri.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa