BARAZA WAZI LA MADIWANI HALMASHAURI YA MJI IFAKARA.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara amewataka wajumbe wa baraza la madiwani kufanya kazi iliyopo mbele yao ili kama kuna mapungufu yaliyojitokeza mwaka wa fedha 20 17/2018 kuimarisha pale palipo kuwa na mapungufu ili mwisho Halmashauri iweze kuwa na tija.
Ameyasema hayo katika baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wakati wakipitia agenda zinazo husu maendeleo ya Halmashauri ikiwemo mradi wa maji na mabomba katindiuka.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara ndugu Gabrieli Malisa amewashukuru wajumbe wote waliohudhuria baraza kwa majadiliano juu ya mustakabali wa halmashauri na kuwapongeze wajumbe wote walioonyesha ushirikiano kwenye shughuli ya kukimbiza mwenge katika halmashauri na mategemeo ya kupata nafasi nzuri.
Aidha baada ya kumalizika kwa agenda zilizokuwa zikijadiliwa kwenye baraza hilo walifanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara kwa kupiga kura ya siri wakiwa tayari wamependekeza majina mawili Mh:Johakimu luselo,Magreti Lipindi na baada ya hapo Mh Magreti Lipindi kutangazwa mshindi kwa kura 08
Hata hivyo madiwani walichagua kamati za kudumu za halmashauri Kamati ya Afya, Uchumi,UKIMWI, Mipango miji,na Kamati ya fedha.
Naye Makamu Mwenyekiti mteule Mh: Magreti Raphael Lipindi amewashukuru wajumbe wote wa baraza na madiwani kwa kumuamini na kumpiga kura nyingi zilizojitosheleza na kwa dhamana waliyompa na kuahidi kutowaangusha, kikubwa ni ushirikiano ili kuweza kufikia malengo ya Halmashauri kama yalivyo pangwa na kufanya vizuri.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa