Madiwani na watendaji kata wa Halmashauri ya mji wametakiwa kuhudhuria vikao vya wananchi na kuhamasisha ulipaji wa kodi ili kuongeza pato na kuleta maendeleo katika Halmashauri.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Ndg. James Ihunjo alipokuwa akitoa hotuba katika Baraza la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Ifakara.
Hilo linajiri baada ya mapato ya Halmashauri ya Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/19 kupungua ukilinganisha na mwaka uliyopita, Ivyo Mkuu wa Wilaya na wajumbe wa Baraza wamaamua kuweka mikakati itakayosaidia kukuza pato la Halmashauri kupitia ukusanyaji Kodi.
Sanjari nahilo Mkuu wa Wilaya amezungumzia upimaji wa Viwanja unaotarajiwa kuanza kabla ya masika ili kutatua migogoro ya Ardhi kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa