Zaidi ya shilingi milioni 240 zinahitajika kuziba mto Lumemo ilikunusuru wananchi zaidi ya 16500 kutoka kata tano za wilayani kilombero walio kumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizokuwa zinanyesha na kupelekea mto huo kuvunja kingozake na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi hao.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lumemo Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya Mji Ifakara Francis Ndulane amewataka wananchi kuwa watulivu wakatiserikali ikiendelea na mchakato kuhakikisha mafuriko hayatokei tena.
Aidha Ndulane amesema mvua hizo zilisababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara milioni 464 zimeshapatikana kwaajili ya kutengeneza barabara huku wathirika wa mafuriko wakipewa viwanja ilikujinusuru na adhahiyo.
Kwaupande wao wananchi ambao ni waathirika wa mafuriko hayo wakiwemo wenyeviti wa vitongoji wameiyomba serikali kuanza matengenezo ya mto huo mapema kabla mvua za vuli hazijaanza kunyesha.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: 0738 223 543
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa